Maisha yetu

Wakenya tumeishi si haba. Tumeishi kuona na kusikia mengi. Katika haya maisha, tumedanganywa kwa mengi. Lakini ijapo haya ndo maisha tuishio, tunamalizana na kuzoeana. Wazee na hata vijana, sote tumeoza vya kutosha. Twaishi kwa matarajio. Twatumbua macho na kutunga mbele kwa ari na hamu na pia manufaa. Tumejaza juhudi na ari moyoni lakini pindi tufanyavyo hivi, kuna wale wana njama nyingine. Hawa hutufanya tujilaumu, tuwalaumu na kuilaumu. Hawa wafanya tuamini yasiyoaminika na tufikapo hapo, twaanza kupekua tukiutafuta ukweli. Jana imepita wenzangu. Imepita na majuto. Leo twajua haipo kwani ina wenyewe. Kesho haijazaliwa na twatumai ardhi yetu itazaa matunda mema. Twataka kuneemesha kila mtoto. Twataka hata wale walio wakimbizi ndani ya ardhi yao wajae tabasamu. Katika haya maisha tuyatamaniyo, lazima tuamke. Lazima tutanabahi na pia tuzinduke.

Popular posts from this blog

I LOVE YOU LORD, GREATER THAN ANYTHING - LIONEL PETERSEN

I know why caged birds sing - Dr. Maya Angelou

Success and the ladder thereof?